Monday, November 10, 2008

NI MIRIAM ODEMBA a.k.a MIMI.Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya urembo(Miss Earth 2008), Miriam Odemba ameibuka mshindi wa pili katika fainali za mashindano hayo zilizofanyikia katika ukumbi wa Clark Expo Ampitheater mjini Pampanga.Mshindi wa kwanza ni Karla Paula Henry kutoka nchini Philippines huku nafasi ya tatu ikienda kwa Miss Mexico,Abigail Elizalde.Mshindi wa nne ni Miss Brazil,Tatiene Alvez.Jumla ya washiriki 84 walishiriki shindano hilo.Kwa niaba ya Wadau na Timu nzima ya WAUKWELI tunapendaa kutoa hongera nyingi kwa Miriam Odemba,kampuni ya Compass Communications chini ya Maria Sarungi na watanzania wote kwa ujumla.
MUNGU IBARIKI AFRICA ,MUNGU IBARIKI TANZANIA.

No comments: