Monday, April 7, 2008

Waukweli amenunua Gari

Jamani eee,Nimenunua gari,Napata tabu sana kuzunguka jijini ila mvua ikinyesha huwa naliacha nyumbani na kuchukua lingine.Asante David kwa kuniuzia gari lako.Baya we unalo.

6 comments:

Anonymous said...

wewe dada unavituko sijapata kuona, hongera mwaya

totoo said...

heheheeeeeeeeee..wewe umeiba jeshi la wapi..mlendi rova huo..??hehe..umeniacha hoi kinoma wangu..

Matty said...

hahahahahahahah Wajina leo umenivunja mbavu sana...wakikuona watalii utapata dili kibao kuwapeleka mbugani wanapenda sana magari hayo!

Anonymous said...

Jamani Matty hili Gari nimenunua juzi ata sijakaa nalo sana,Nitaenda kupata dili Ngorongoro.

We totoo,Sijaiba bwana nimeuziwa na kaka mmoja anaitwa David sasa sijui yeye ameiba ahahaha..,Ila sijawai kamatwa na Trafic.
WAUKWELI.

Waukweli said...

Kuna mtu kanijibia hapo juu,Haya yote heri ili mradi usitukane.
Totoo sijaiba nimenunua bwana wananitambua jijini,Ukija Dar ntakupa lifti kima wangu.

Matty wajina usijali sina muda mrefu ntalipeleka ngorongoro nikapate mapesa.Si unajua vitu kama hivi ni dili kule.
WAUKWELI.

Mtized said...

Mbona naona kuna mdau ameitwa Kima hapa? Au ndiyo namna mpya ya kuita watu huko Bongo sikuhizi?